Mfumo mpya wa biashara ya nje ya China umeleta maendeleo mapya (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 03, 2021
Mfumo mpya wa biashara ya nje ya China umeleta maendeleo mapya
Matrekta ya uhandisi yako tayari kusafirishwa nchi za nje kutoka Bandari ya Yantai, Mkoa wa Shandong ulioko Mashariki mwa China, Tarehe 28, Novemba, Mwaka 2021,. (Tovuti ya People’s Daily/Tang Ke)

Ripoti ya Mpango wa 14 wa Miaka Mitano wa Maendeleo Bora ya Biashara ya Nje (2021-2025) iliyotolewa hivi karibuni na Wizara ya Biashara ya China inasema kwamba, mwaka huu wa 2021 thamani ya biashara za bidhaa na huduma ya China imekuwa kubwa zaidi duniani, na wenzi wa biashara wametapakaa katika nchi na maeneo 230 duniani.

Ripoti hiyo ilisema, katika miaka mitano iliyopita, yaani kipindi cha “Mpango wa 13 wa miaka mitano ya maendeleo ya uchumi na jamii”, China ilichangia asilimia 34.9 katika ongezeko la uagizaji bidhaa wa Dunia nzima.

Ripoti hiyo inaeleza zaidi kwamba, mwaka huu ni mwaka wa kwanza wa “Mpango wa 14 wa miaka mitano”. Kwa kuwa hali ya kimataifa na nchini China ilikumbwa na changamoto kubwa, ongezeko la kasi ya biashara ya nje ya China lililopatikana mwaka huu ni matunda ya juhudi zisizo rahisi.

Katika miezi 10 ya kwanza ya Mwaka 2020, jumla ya uagizaji na uuzaji nje wa bidhaa wa China ulifikia dola za kimarekani trilioni 4.89, ikiwa ni ongezeko la asilimia 31.9 mwaka hadi mwaka. Kiasi hicho ni kikubwa zaidi kuliko kile cha mwaka mzima uliopita na kuweka rekodi mpya. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha