Ndani ya Bustani ya Shougang: Utulivu kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 03, 2021
Ndani ya Bustani ya Shougang: Utulivu kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi
Picha iliyopigwa Novemba 30, 2021, ikionesha mandhari mbalimbali za Bustani ya Shougang katika Wilaya ya Shijingshan, Beijing. (People's Daily Online/Peng Yukai)

Bustani ya Shougang, ni eneo la kinu cha chuma lililogeuzwa kuwa Maeneo yenye shughuli za Kitamaduni na Michezo katika Wilaya ya Shijingshan Magharibi mwa Beijing.

Kwa sasa imekuwa Makao Makuu ya Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi kwa Walemavu ya Beijing Mwaka 2022.

Aidha, eneo hilo limekuwa na maeneo mengine ya michezo yaliyoanza kujengwa Mwaka 2016 na sasa baadhi yao yanatazamiwa kutumika kwenye michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2022.

Shougang iliyojengwa Mwaka 1919, ikimaanisha "kiwanda cha chuma cha mji mkuu" kwa lugha ya Kichina, ni ishara ya historia ya sekta ya viwanda ya China. Baada ya kuingia Karne ya 21, Shougang ilihamishiwa katika Mkoa jirani wa Hebei mnamo Mwaka 2010, na eneo hilo kubwa liliorodheshwa katika kundi la kwanza la orodha ya uhifadhi wa urithi wa viwanda wa China.

Mabaki ya karakana za zamani za ukarabati, mtambo wa kuyeyusha, na tanuri yamekuwa "kumbukumbu ya chuma" ya zamani, wakati maeneo mapya ya michezo ya barafu na theluji, kama vile majukwaa ya kuruka juu ya theluji, sasa yameanza kuvutia ufuatiliaji wa watu.

Kadri Mashindano ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Mwaka 2022 yanapokaribia, Bustani ya Shougang iko tayari kukaribisha wanamichezo kutoka duniani kote, watakapokutana jijini Beijing kwa ajili ya kushiriki katika mashindano hayo. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha