Uwanja wa zamani wa mashindano ya mbio ya Farasi wakutana na Reli ya Mwendo kasi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2021
Uwanja wa zamani wa mashindano ya mbio ya Farasi wakutana na Reli ya Mwendo kasi

Jumapili ya wiki iliyopita, treni ya mwendo kasi iliingia Kituo cha Uwanja wa mashindano ya mbio ya Farasi wa Shandan kwenye Reli ya mwendo kasi ya Lanzhou-Xinjiang. 

Siku hiyo Kituo cha Uwanja wa mashindano ya mbio ya Farasi wa Shandan kwenye Reli ya mwendokasi ya Lanzhou-Xinjiang, ambacho kina urefu wa zaidi ya mita 3000 kutoka usawa wa bahari, kilianza kutoa huduma ya usafiri wa abiria.

Kituo hicho kiko kwenye Wilaya ya Shandan, Mji wa Zhangye, Mkoa wa Gansu. Kituo hicho hakikuwa na huduma ya usafiri wa abiria. Mwezi Machi wa mwaka huu, mradi wa ukarabati na upanuaji ulianzishwa katika kituo hicho, ukiwa na nyumba mbili za abiria zenye mita za mraba 1080, maeneo mawili ya abiria kupanda treni na vifaa vingine husika. Baada ya kuzinduliwa rasmi, treni nyingi husimama kwenye kituo hicho kila siku. Abiria wanaweza kupanda treni hizo kwenda miji ya Lanzhou, Xi’an, Urumqi, Jiayuguan, Dunhuang n.k.

Uwanja wa mashindasno ya mbio ya Farasi wa Shandan ni moja kati ya viwanja hivyo vyenye historia ndefu zaidi duniani. Tokea Enzi ya Han (K.K. 202-B.K. 220), eneo hilo lilikuwa ni kituo cha kiserikali cha kufuga farasi. Tangu Jamhuri ya Watu wa China ianzishwe, uwanja huo ulikuwa umewafuga farasi kwa ajili ya jeshi karibu kwa muda wa nusu karne.

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na ufanisi mkubwa wa kazi ya kulinda mazingira ya asili ya Mlima Qilian, uwanja huo wa Farasi ulianza kukuza shughuli za utalii kwenye mazingira ya asili. Baada ya Kituo cha treni cha Shandan kufunguliwa itakuwa rahisi kwa watalii kutembelea mandhari ya kipekee ya milima ya theluji, mbuga, na farasi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha