Mfumo ulioboreshwa wa uchaguzi wa Hong Kong unalenga wingi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2021
Mfumo ulioboreshwa wa uchaguzi wa Hong Kong unalenga wingi
Kitabu cha Historia ya Ushiriki wa Hong Kong katika Mageuzi na Ufunguaji mlango wa China kikizinduliwa katika hafla iliyofanyika Hong Kong, Mkoa wa Utawala Maalum wa China, Desemba 6, 2021.(Xinhua/Lui Siu Wai)

HONG KONG - Xia Baolong, Mkuu wa Ofisi ya Masuala ya Hong Kong na Macao wa Baraza la Serikali ya China amesema Kanuni ya "wazalendo watawala Hong Kong" ni msingi wa utekelezaji thabiti na endelevu wa sera ya "nchi moja, mifumo miwili,"

"Kuchagua wazalendo kutawala Hong Kong hakulengi umoja, bali wengi," Xia amesema Jumatatu ya wiki hii katika hotuba yake ya video kwenye uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Ushiriki wa Hong Kong katika Mageuzi na Ufunguaji mlango wa China.

Amesema, mwitikio kutoka kwa jamii kuhusu uchaguzi wa awamu ya saba wa Baraza la Kutunga Sheria (LegCo) katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) unaonyesha kikamilifu sifa za uwakilishi mpana, ushirikishwaji wa kisiasa, ushiriki wenye uwiano na ushindani wa haki chini ya mfumo ulioboreshwa wa uchaguzi.

Pia amesisitiza kuwa mfumo wa uchaguzi wa HKSAR ni mambo ya ndani ya Jamhuri ya Watu wa China ambayo hayaingiliwi kati na nchi nyingine.

"Watu wa China wana imani kuhusu demokrasia ya ujamaa wenye umaalum wa China na mfumo wa demokrasia unaolingana na hali halisi ya HKSAR," ameongeza.

Kwa upande wake, Carrie Lam, Mtendaji Mkuu wa HKSAR, amesema Hong Kong siyo tu imetoa mchango mkubwa katika mageuzi na ufunguaji mlango lakini pia imefaidika na maendeleo ya haraka ya China Bara.

Ameelezea majukumu mengi ya Hong Kong katika mageuzi na ufunguaji mlango wa uchumi wa China kama shahidi, mshiriki, mchangiaji na mnufaika.

Katika uzinduzi huo, pia mkataba wa ushirikiano kati ya Eneo la Ghuba ya Guangdong-Hong Kong-Macao ulitiwa saini. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha