Jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji la Bustani ya Shougang laanza kutengeneza theluji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 13, 2021
Jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji la Bustani ya Shougang laanza kutengeneza theluji
Jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji la Bustani ya Shougang likianza rasmi kutengeneza theluji. Mpiga picha: Li Qiang

Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, alfajiri ya Jumatatu (leo), mashine nne za kutengeneza theluji, taa za usiku za jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji zimewashwa, hali ambayo inaonesha utoaji wa umeme kwenye uwanja huo wa michezo umefikia kigezo cha matumizi wakati wa mashindano, na jukwaa la kuteleza na kuruka kwenye theluji la Bustani ya Shougang limeanza rasmi kutengeneza theluji.

Jukwaa la kuteleza na kuruka juu ya theluji la Bustani ya Shougang liko ndani Bustani mpya ya Shougang katika Eneo la Shijinshan la Beijing. Ni uwanja pekee wa mashindano ya kwenye theluji hapa Beijing kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya Mwaka 2022. Litatumika kwa mashindano ya aina mbili: mruko juu ya theluji kwa mtindo huru na kutumia ubao kuteleza na kuruka kwenye theluji. Baada ya kumalizika kwa michezo hiyo, utakuwa uwanja wa kwanza duniani unohifadhiwa na kutumika kwa kuruka juu ya theluji, ulio wazi kwa umma. 

Kazi ya kutengeneza theluji ni moja ya maandalizi muhimu kabla ya mashindano kuanza rasmi. Kiasi cha jumla cha utengenezaji wa theluji ni mita za ujazo 6,500 hivi. Utengenezaji wa theluji umegawanyika katika hatua nne: kutengeneza theluji, kulimbikiza theluji, kujenga njia za kutelezea na kukarabati njia za kutelezea. Hatua zote za utengenezaji wa theluji zimekamilishwa na wataalamu wanane na mashine 11 za hali ya juu zilizofungwa kwenye eneo hilo.  

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha