

Lugha Nyingine
China yaweka mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uchumi ya Mwaka 2022 kwa sera thabiti
BEIJING - Wakati Mkutano Mkuu wa mwaka wa Kazi ya Uchumi wa Taifa la China ukihitimishwa Beijing, China Ijumaa ya wiki iliyopita ambapo ulizingatia juhudi za kudumisha utulivu wa nchi wakati wa kutafuta maendeleo, viongozi wakuu wa China wamepanga vipaumbele vya kazi ya uchumi ya mwaka ujao.
Katika hotuba yake kwenye mkutano huo, Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, alipitia kazi ya uchumi ya nchi kwa Mwaka 2021, kuchambua hali ya sasa ya uchumi na kupanga kazi ya mwaka ujao.
Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Wang Huning, Zhao Leji na Han Zheng, ambao ni wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, walihudhuria mkutano huo wa siku tatu.
Maendeleo Imara
Kwa mujibu wa mkutano huo, kazi ya uchumi ya mwaka ujao inapaswa kutoa kipaumbele katika utulivu wa nchi wakati wa kutafuta maendeleo.
Mkutano huo umesema kwamba, hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kulinda uthabiti wa uchumi wa jumla, kudumisha viwango muhimu vya uchumi ndani ya safu inayofaa na kulinda utulivu wa jamii ili kujiandaa kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC
.
Umeeleza zaidi kwamba, Mwaka 2021 umekuwa hatua muhimu kwa Chama na Taifa, ambapo China imeongoza katika maendeleo ya uchumi na udhibiti wa janga la virusi vya korona duniani, na maendeleo yaliyopatikana katika nguvu za kisayansi, unyumbufu wa mnyororo wa viwanda, mageuzi na ufunguaji mlango, kipato cha watu na ustaarabu wa ikolojia.
Hata hivyo, mkutano huo umetahadharisha kuwa maendeleo ya uchumi ya China yanakabiliwa na shinikizo kutokana na upungufu wa mahitaji, matukio yanayoathiri ugavi na matarajio yanayopungua, na mazingira ya nje yanazidi kuwa magumu, mabaya na kutokuwa na uhakika.
Mkutano huo ulisisitiza uongozi wa Kamati Kuu ya CPC, kukuza maendeleo ya kiwango cha juu na kutafuta maendeleo huku kukihakikisha utulivu wa nchi.
Waraka wa Sera wa Mwaka 2022
Mkutano huo umeeleza kwamba, China itaendelea kutekeleza sera za utendaji za mambo ya fedha na sera madhubuti za fedha ili kuhimiza maendeleo tulivu ya uchumi mwaka ujao.
Mkutano umeahidi kutekeleza sera mpya za kupunguza ushuru na ada, kuimarisha uungaji mkono kwa biashara ndogo na za kati, ujasiliamali mdogo, sekta ya viwanda na utatuzi wa hatari, na kuendeleza uwekezaji wa miundombinu kwa nguvu mwafaka.
Umebainisha kwamba, vipaumbele vya kiuchumi vya mwaka ujao pia ni pamoja na kuimarisha maendeleo kupitia sera za mageuzi na ufunguaji mlango, kukuza usawa na uratibu wa maendeleo ya kikanda, na kuhakikisha kwamba sera zake za kijamii zinalinda vyema maslahi ya watu.
Aidha, mkutano umezingatia juhudi katika kuongeza ajira kwa vijana, wakiwemo wahitimu wa vyuo vikuu, na kuboresha sera za ajira na hifadhi ya jamii.
Kwa mujibu wa takwimu za Serikali, katika miezi 10 ya kwanza ya Mwaka 2021, China iliongeza nafasi mpya za ajira milioni 11.33 katika maeneo yake ya mijini, na kufikia lengo lake la mwaka mzima mapema.
Huku mkutano ukirejelea kanuni kwamba "nyumba ni ya kuishi, siyo ya kubahatisha," mkutano huo ulisema China itaunga mkono soko la nyumba ili kukidhi mahitaji ya wanunuzi wa nyumba na kupitisha sera mahususi kwa miji ili kuongeza mzunguko mzuri na maendeleo bora ya sekta hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma