China, Russia zimepata mafanikio mapya katika uratibu wa kimkakati, ushirikiano wa vitendo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 15, 2021
China, Russia zimepata mafanikio mapya katika uratibu wa kimkakati, ushirikiano wa vitendo
Rais wa China Xi Jinping akifanya mazungumzo na Rais wa Russia Vladimir Putin kwa njia ya video mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Juni 28, 2021. (Xinhua/Ding Lin)

MOSCOW - Rais wa China Xi Jinping atafanya mkutano na mwenzake wa Russia Vladimir Putin kwa njia ya video siku ya Jumatano (leo), ikiwa ni mkutano wa pili wa mtandaoni kwa mwaka huu tangu ule wa awali uliofanyika Juni 28.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, China na Russia zimechukua maadhimisho ya miaka 20 tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Ujirani Mwema na Ushirikiano wa Kirafiki kati ya China na Russia kuwa ni mwanzo mpya wa kuhimiza uratibu wa kimkakati na ushirikiano wa kina wa kivitendo kati ya pande hizo mbili.

Mafanikio mapya yamepatikana katika nyanja za siasa, uchumi na biashara, sayansi na teknolojia, nishati na kijeshi.

Wakuu wa nchi hizo wamedumisha mawasiliano ya mara kwa mara na ya karibu kwa Mwaka 2021. Mwezi Mei mwaka huu, Xi na Putin walishuhudia uzinduzi wa mradi wa ushirikiano wa nishati ya nyuklia wa pande mbili kwa njia ya video.

Mwezi Juni, marais hao walikutana kwa njia ya video ili kutangaza kwa pamoja kuongeza muda wa Mkataba wa Ujirani Mwema na Ushirikiano wa Kirafiki kati ya China na Urusi.

Mwezi Julai, Xi alituma salamu za rambirambi kwa Putin kutokana na ajali ya ndege ya abiria ya Russia. Mwezi Agosti, wakuu hao walifanya mazungumzo kwa njia ya simu kujadili uhusiano kati ya nchi hizo mbili na hali ya Afghanistan.

Huku China ikiwa mwenzi mkubwa wa kibiashara wa Russia kwa miaka mingi mfululizo, thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili ilizidi dola za Marekani bilioni 100 mwaka 2018 kwa mara ya kwanza na imedumisha kasi hiyo licha ya janga la UVIKO-19.

Takwimu rasmi zinaonesha kwamba, katika miezi 10 ya kwanza ya mwaka huu, biashara ya bidhaa kati ya China na Russia ilifikia dola za kimarekani bilioni 115.6, na kuzidi thamani ya biashara ya mwaka mzima wa 2020.

Mwezi Machi, China na Russia zilitia saini makubaliano kuhusu kujenga kwa pamoja kituo cha kimataifa cha utafiti wa sayansi kuhusu mwezi.

Mwaka wa Uvumbuzi wa Kisayansi na Kiteknolojia kati ya China na Russia ulihitimishwa mwezi uliopita, ambao ulishuhudia matukio zaidi ya 1,000 kuhusu uvumbuzi na ushirikiano wa kisayansi.

Sehemu nambari 7 na 8 za kinu cha nyuklia cha Tianwan na sehemu nambari 3 na 4 za kinu cha nyuklia cha Xudapu zilianza kujengwa Mwezi Mei, ambao ni mradi mkubwa zaidi wa pamoja wa China na Russia katika sekta ya nishati ya nyuklia

Zoezi la pamoja la kijeshi kati ya China na Russia la ZAPAD/INTERACTION-2021, lilifanyika Kaskazini Magharibi mwa China. Majeshi ya majini kutoka nchi hizo mbili yaliendesha safari yao ya kwanza ya baharini, na vikosi vya anga vilifanya doria yao ya tatu ya kimkakati ya angani.

Wanajeshi kutoka majeshi hayo mawili waliimarisha uratibu kwa kushiriki katika zoezi la kijeshi la "Misheni ya Amani 2021" ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai (SCO) na Michezo ya Kimataifa ya Majeshi ya Mwaka 2021.

“Zikiwa wenzi wa kina wa uratibu katika zama mpya, China na Russia zinasaidiana kithabiti katika masuala makuu yanayohusu maslahi ya kimsingi ya kila upande, kuratibu kwa karibu mambo ya kimataifa, na kuchukua jukumu muhimu katika kudumisha amani na utulivu wa kimataifa” Balozi wa China nchini Russia Zhang Hanhui amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha