Naibu Waziri Mkuu wa China ataka juhudi kuhakikisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi "rahisi, salama na ya kifahari" (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 16, 2021
Naibu Waziri Mkuu wa China ataka juhudi kuhakikisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi
Naibu Waziri Mkuu wa China Han Zheng, ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkuu wa kikosi kazi kinachosimamia maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022, akizungumza na wafanyakazi wakati alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuogelea cha Beijing, Mji Mkuu wa China, Desemba 14, 2021. (Xinhua/Pang Xinglei)

BEIJING - Naibu Waziri Mkuu wa China Han Zheng amesisitiza haja ya kuweka kipaumbele katika kuzuia na kudhibiti janga la UVIKO-19 ili kufanikisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Mwaka 2022 "rahisi, salama na ya kifahari".

Han, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkuu wa kikosi kazi kinachosimamia maandalizi ya Michezo ya Omlimpiki ya Mjira ya Baridi ya Beijing 2022, amesema hayo Jumanne ya wiki hii wakati wa ziara ya ukaguzi wa viwanja kadhaa huko Beijing, ukiwemo Jumba la Taifa la Mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye barafu. Kijiji cha Olimpiki ya Majira ya Baridi, Kituo Kikuu cha Vyombo vya Habari, Jumba la Taifa la Michezo na Kituo cha Taifa cha Kuogelea.

Han amesema kuwa janga hilo ni mtihani mkali kwa waandaaji wa michezo hiyo, na amehimiza kila mtu kukaa macho wakati wote na kufuatilia kwa uangalifu hatua za kukabiliana na UVIKO-19.

Huku zikiwa zimesalia siku 50 pekee kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi kuanza, Han pia ametoa mwito wa juhudi madhubuti katika maandalizi ya mwisho kwenye kumbi na vifaa vingine ili kuhakikisha michezo hiyo inafanyika vizuri.

Han amesisitiza kuwa mbali na kuandaa mashindano hayo makubwa ya michezo, kumbi hizo pia zinapaswa kukidhi mpango wa China wa "Kujenga Afya kwa wote", na kuhudumia umma baada ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi.

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 itafanyika kati ya Februari 4 na 20, ikifuatiwa na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu kuanzia Machi 4 hadi 13.

Mji Mkuu wa China, Beijing unatazamiwa kuwa mji wa kwanza kuandaa Michezo ya Olimpiki ya majira ya joto na ya baridi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha