Bustani ya Wanyama ya Chongqing yafanya hafla ya kuwapa majina mapacha wa panda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 23, 2021
Bustani ya Wanyama ya Chongqing yafanya hafla ya kuwapa majina mapacha wa panda
Pacha wa panda "Xingxing" na "Chenchen" wanaonekana kwenye Bustani ya Wanyama ya Chongqing katika mji wa Chongqing ulioko Kusini Magharibi mwa China, Desemba 21, 2021. Bustani ya Wanyama ya Chongqing imefanya hafla ya kuwapa majina mapacha wa panda "Qizhen" na "Qibao", na "Xingxing" na "Chenchen" siku ya Jumatano ya wiki hii. Pacha wa panda ambao ni kaka na dada "Qizhen" na "Qibao" walizaliwa katika bustani hiyo Septemba 13 mwaka huu, majina yao kwa pamoja yanamaanisha "watoto wa thamani". Pacha wengine wa panda, waliozaliwa Juni 10 mwaka huu wameitwa "Xingxing" na "Chenchen". (Xinhua/Tang Yi)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha