Xi’an Yaimarisha zaidi Udhibiti wa Maambukizi ya Virusi vya Korona

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 24, 2021
Xi’an Yaimarisha zaidi Udhibiti wa Maambukizi ya Virusi vya Korona
(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Kuanzia saa sita usiku wa Tarehe 23, maeneo ya makazi yote (vijiji vyote) na mashirika yote ya kote mjini Xi’an, Mkoa wa Shaanxi nchini China yameanza kutekeleza hatua za kujitenga kijamii ili kukabiliana na mlipuko wa Virusi vya Korona.

Taarifa ya Serikali ya Mji wa Xi’an inaeleza kuwa, katika kila familia, mtu mmoja anaruhusiwa kwenda nje kununua mahitaji muhimu kila baada ya siku mbili, huku wanafamilia wengine wakibaki nyumbani kutotoka nje, mbali na wale wanaofanya kazi ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona, watoa huduma za uendeshaji wa mji au kulinda maisha ya raia. Uthibitisho wa ruhusa kutoka shirika au mtaa unahitajika ili kutoka nje. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha