

Lugha Nyingine
China Yarusha Setilaiti Mbili Mpya za majaribio kwenye Anga la Juu (2)
Alhamisi ya wiki hii, China imerusha Roketi ya Changzheng No.7 A, ambayo imepeleka setilaiti mbili kwenye anga la juu.
Roketi ilirushwa saa 12 na dakika 12 mchana kwa saa za Beijing kwenye Uwanja wa Kurusha Roketi wa Wenchang, ulioko Kusini mwa Mkoa wa Hainan. Punde ilizipeleka setilaiti “Shiyan-12 01” na “Shiyan-12 02” kwenye obiti iliyopangwa.
Neno la Kichina la“Shiyan”, maana yake ni “jaribio”. Shirika la Sayansi na Teknolojia ya Anga la Juu la China, ambalo lilitengeneza setilaiti hizo mili lilisema, setilaiti hizo zitafanya uchunguzi kuhusu mazingira ya anga la juu na majaribio mengine husika ya kiteknolojia.
Roketi hiyo ya kubeba satelaiti ni roketi ya aina ya Changzheng No.7 iliyorekebishwa upya, ikiwakilisha roketi za kizazi kipya za China za obiti ya kiwango cha juu zenye ukubwa wa kati. Imegawanyika katika ngazi tatu na ina urefu wa mita 60.7, ambayo ni roketi ndefu zaidi ya China inayofanya kazi sasa. Na hii ni mara ya 402 kwa roketi ya Changzheng kupeleka setilaiti kwenye anga la juu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma