

Lugha Nyingine
Sheria ya Marekani kuhusu Xinjiang ni ukandamizaji wa kiuchumi, kinyume na sheria za Kimataifa - Wachambuzi
BEIJING – Wachambuzi wameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba, Marekani kutia saini kile kinachoitwa "Sheria ya Kuzuia Kulazimishwa kufanya kazi kwa Wauyghur" kuwa sheria ambayo inapiga marufuku uagizaji bidhaa kutoka eneo la Xinjiang nchini China ni ukandamizaji wa kiuchumi na jaribio jingine la kuingilia mambo ya ndani ya China.
Sheria hii, inayotokana na habari zisizo sahihi na zenye nia mbaya dhidi ya China, ni "uingiliaji mkubwa wa mambo ya ndani ya China na ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa," amesema Muhammad Asif Noor, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Amani na Kidiplomasia yenye makao yake mjini Islamabad, Pakistan. .
Noor amesema, sera ya mambo ya nje ya Marekani imekuwa ikiegemea kuingilia mambo ya ndani ya nchi mbalimbali, lakini Dunia si kipofu tena.
Abdul-Raziq Ziyada, mchambuzi wa kisiasa wa Sudan, anaona uamuzi wa Marekani ni kama "ukiukaji wa wazi wa sheria ya kimataifa inayosimamia uhusiano kati ya nchi".
Kwa mujibu wa Cavince Adhere, mtaalam wa uhusiano wa kimataifa kutoka nchini Kenya, kusainiwa kwa sheria hiyo ni "kuendeleza upotoshaji wa muda mrefu wa Marekani juu ya Wachina wanaoishi Xinjiang na jaribio la wazi la kuweka siasa kwenye uhusiano wa kiuchumi" kati ya China na Marekani.
“Vikwazo vya serikali ya Marekani dhidi ya Xinjiang vinaweza kusababisha hali ambayo wafanyabiashara na wanunuzi wa bidhaa wa Marekani na China lazima wakabiliane na athari za "siasa zenye sumu" badala ya kunufaika na utandawazi wa uchumi” Adhere amesema.
Rais wa Kituo cha Uchambuzi cha Russia na China Sergei Sanakoyev anaamini kuwa masuala yanayohusiana na Xinjiang si masuala ya haki za binadamu hata kidogo, bali ni masuala ya kupambana dhidi ugaidi na makundi yenye harakati za kujitenga.
Wakati Marekani ilipoishutumu China kwa "kulazimisha kufanya kazi", haikutoa ushahidi wowote wa kuridhisha, amesema, na kuongeza kuwa jaribio la Marekani ni kuibua migogoro kati ya makabila mbalimbali na dini tofauti nchini China, kuyumbisha hali ya utulivu na kuzuia maendeleo ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma