

Lugha Nyingine
Picha: Pilikapilika za Uvuvi wa Majira ya Baridi Kwenye Ziwa Chagan
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2021
Ziwa Chagan liko kwenye Wilaya inayojiendesha ya kabila la Wamongolia Qian Gorlos, Mji wa Songyuan, Mkoa wa Jilin, China. Ziwa hilo lina samaki wengi wa aina mbalimbali likisifiwa kuwa “Kabila la Mwisho la Uvuvi na Uwindaji la Kaskazini mwa China”. Kila mwishoni mwa Desemba, wavuvi hutoboa mamia ya matundu kwenye barafu iliyoganda juu ya ziwa hilo, halafu kutumia matundu hayo kuzungusha wavu wa kunasia samaki wenye urefu wa mita maelfu. Mwishowe wavuvi hutumia farasi kuvuta winchi ili kufunga wavu na kuvua samaki. Maajabu ya nyavu za winchi za uvuvi katika Ziwa Chagan yamejumuishwa kwenye orodha ya Urithi wa kitaifa wa Utamaduni usioshikika wa China. (Picha/Yan Linyun kutoka Xinhua)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma