Misri yakamata Sarafu na Kinara cha Kale cha Mshumaa kwenye Uwanja wa Ndege

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 06, 2022
Misri yakamata Sarafu na Kinara cha Kale cha Mshumaa kwenye Uwanja wa Ndege
Mkusanyiko wa picha ukionesha sarafu za kale zilizokamatwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Cairo, Misri, Januari 5, 2022. (Picha/Xinhua)

Idara ya Utafiti wa Mabaki ya Kale ya Misri na polisi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo Jumatano ya wiki hii walikamata sarafu tisa za kale na kinara kimoja cha kale cha mshumaa cha shaba ya kimanjano, ambavyo abiria mmoja alijaribu kuvisafirisha kwa magendo kwenda nchi za nje.

Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kwenye taarifa yake ilisema, sarafu hizo za dhahabu na fedha zinatoka zama tofauti za Misri ya Kale, zikiwemo Ptolemaic, Byzantine na Ugriki.

Imeongeza kuwa, “Mchakato wa ukaguzi na uchambuzi umethibtisha sarafu hizo ni mabaki ya kale na zinalindwa kwa mujibu wa 'Sheria ya Uhifadhi wa Mambo ya Kale' ya Mwaka 1983.”

Taarifa hiyo pia ilisema, “Tutachukua hatua zote za kisheria kwa tukio hilo.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha