Treni ya Michezo ya Olimpiki Yaonekana kwenye Kituo cha Chongli cha Reli ya Beijing-Zhangjiakou

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 07, 2022
Treni ya Michezo ya Olimpiki Yaonekana kwenye Kituo cha Chongli cha Reli ya Beijing-Zhangjiakou

Januari 6, Treni ya G9981 ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing yakisimama kwenye Kituo cha Chongli cha Reli ya Beijing-Zhangjiakou.

Habari zinasema, treni zote za michezo hiyo zitakuwa ni za mwendo kasi za Fuxing, ambazo kasi zao zinafikia kilomita 350 kwa saa, na ndani ya treni kuna studio za 5G. Kwa jumla kutakuwa na treni 8 za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, na kila treni itaweza kupokea abiria 564. Muonekano wa kila treni ni picha zinazoonesha mada ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi.

Treni za Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing zitafanya usafiri kuanzia Januari 21 hadi Machi 16. Wakati huo kila siku unapangwa usafiri wa treni 40 za kwenda na kurudi, kimsingi, kila siku kuna usafari wa treni 17, na kuna usafari wa treni 23 za ziada ambazo zitatumika wakati zinapohitajika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha