Hali ya Soko la Reli ya Maeklong la Thailand chini ya athari za maambukizi ya virusi vya korona

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 07, 2022
Hali ya Soko la Reli ya Maeklong la Thailand chini ya athari za maambukizi ya virusi vya korona

Soko la Reli ya Maeklong liko kwenye Wilaya ya Maekong ya Mkoa wa Samut Khan ulioko eneo la kati la Thailand. Kila siku, kuna treni inayoondoka kutoka Kituo cha Maeklong na kupita kati ya soko hilo. Wauzaji wanaweka vibanda vyao kwenye pande mbili za reli na kuvisogeza kabla ya treni kufika kila mara. Hali hii ilikuwa inavutia watalii wengi kuja soko hilo. Baada ya kutokea kwa maambukizi ya virusi vya korona, idadi ya wasafiri imepungua, na treni zinazopita hapa pia zimepunguzwa kutoka usafiri wa treni nane kuwa usafiri wa treni mbili kwa siku. Wauzaji walioko karibu bado wameshikilia kuuza vitu kwenye kando za reli wakisubiri soko hilo kurejea tena katika hali ya pilikapilika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha