Kazi ya upimaji wa virusi vya korona kwa watu wote wa Tianjin yaanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 10, 2022
 Kazi ya upimaji wa virusi vya korona kwa watu wote wa Tianjin yaanza

Ili kuhakikisha usalama wa maisha na afya ya umma na kuzuia kuenea zaidi kwa virusi vya korona aina ya Omicron, Kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ya Mji wa Tianjin, kikundi cha uongozi cha ukingaji na udhibiti wa virusi vya korona, na Makao makuu ya ukingaji na udhibiti wa virusi vya korona ya Tianjin, viliamua kufanya kazi ya upimaji wa virusi vya korona kwa watu wote mjini humo kuanzia saa moja asubuhi Januari 9.

Hivi sasa, maeneo ya Jinnan, Nankai, Dongli, Xiqing yanafanya kazi ya upimaji kwa utaratibu, na yanatarajiwa kumaliza kazi ya upimaji wa virusi vya korona kwa watu wote wa maeneo hayo ndani ya masaa 24 kutoka saa moja asubuhi ya Januari 9.

Maeneo 12 mengine ya Tianjin pia yataanza kazi ya upimaji wa virusi vya korona kwa mfululizo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha