Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi yachochea uwekezaji wa kampuni za kigeni za michezo nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 10, 2022
Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi yachochea uwekezaji wa kampuni za kigeni za michezo nchini China
Mfanyakazi akitoa maelezo kwa mteja kuhusu vifaa vya mchezo wa kuteleza kwenye theluji katika duka la chapa ya Nordica mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Januari 6, 2022. (Xinhua/Chen Zhonghao)

BEIJING – Kufuatia kufungua duka jipya katika Kituo cha Michezo ya Barafu mjini Beijing, chapa ya vifaa vya mpira wa magongo kwenye barafu ya Marekani TRUE imekaribishwa sana na vijana wanaojifunza mchezo huo.

Duka hilo lililofunguliwa Oktoba 2021, linatoa huduma za manunuzi ya vifaa "vyote kwa pamoja" kwa vijana wanaojifunza mchezo huo katika kituo hicho ili wasilazimike kwenda maeneo mengine mjini Beijing kutafuta moja ya vifaa vya mchezo huo kama vile helmeti, glavu, sketi na vijiti.

"Kwa hivyo soko la China la vifaa vya michezo ya msimu wa baridi linalosukumwa na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing litakuwa na mustakabali mzuri kwa kampuni za kigeni," Wang Zhiyong, Meneja wa Idara ya Kimataifa wa Klabu ya Hockey ya Mji Mkuu wa Beijing.

Ripoti ya utafiti ya Mwaka 2021 kuhusu sekta zinazohusu barafu na theluji za China ilionesha kuwa thamani ya biashara inayotokana na sekta hiyo iliongezeka kutoka yuan bilioni 270 (sawa na dola za kimarekani bilioni 42 za Marekani) Mwaka 2015 hadi yuan bilioni 600 (sawa na dola za kimarekani bilioni 94) Mwaka 2020.

Kwa mujibu wa mpango wa maendeleo wa michezo ya barafu na theluji wa Mwaka 2016 hadi 2025 wa China, thamani ya jumla ya biashara katika sekta hiyo itafikia yuan trilioni 1 ifikapo Mwaka 2025.

Li Yanli, Profesa wa Chuo Kikuu cha Michezo cha Beijing, anasema kuwa, kufanikiwa kwa China kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing imekuza sana maendeleo ya sekta ya barafu na theluji ya China.

Katika Duka la WF Central, jengo kubwa la maduka katikati mwa Jiji la Beijing, daraja la korido kwenye ghorofa ya tatu limejaa bidhaa kutoka zaidi ya chapa 10 za michezo ya majira ya baridi duniani, zikiwemo Bogner, Burton, na Mons Royale.

Zhou Peng, ambaye anafanya kazi katika duka la Bogner katika jengo hilo la maduka, amesema duka hilo lilifunguliwa Desemba, 2021.

"Maeneo mengi ya michezo ya kuteleza kwa kasi kwenye theluji yalipofunguliwa, moja ya aina ya suti za michezo ya kuteleza kwenye theluji ziliuzwa zote kwa muda mfupi," Zhou anasema.

Kwa mujibu wa takwimu kuhusu maeneo ya michezo nchini China za Mwaka 2020 zilizotolewa na Idara ya Taifa ya Michezo ya China, hadi kufikia Desemba 31, 2020, kulikuwa na maeneo 1,888 ya michezo ya barafu na theluji nchini. Inakadiriwa kuwa idadi hiyo itafikia 2,900 mwaka huu wa 2022. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha