WHO yasifia mpango wa kukabiliana na UVIKO-19 wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 10, 2022
WHO yasifia mpango wa kukabiliana na UVIKO-19 wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing
Mhudumu wa treni akionesha zawadi za ukumbusho wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 kwenye treni ya reli ya kasi ya Beijing-Zhangjiakou Desemba 30, 2021. (Xinhua/Huang Zhen)

SINGAPORE – Mtaalam Mwandamizi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Michael Ryan amesema kwamba, Mipango ya Beijing ya kuhakikisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya 2022 mwezi ujao inafanyika kwa usalama wakati wa janga la UVIKO-19 inaonekana kuwa imara.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Lugha ya Kichina nchini Singapore cha Lianhe Zaobao, Mkurugenzi wa Mambo ya Dharura wa WHO Michael Ryan amesema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita.

Ryan amesema kwamba, shirika hilo limefanya kazi na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kutoa ushauri wa kiufundi kuhusu uandaaji salama wa michezo hiyo.

"Viongozi wa China wana hatua kali sana (dhidi ya UVIKO-19), na wametoa mfululizo wa vitabu tofauti vya mwongozo (kuhusu udhibiti wa UVIKO-19)," Ryan amenukuliwa akisema.

"Nina imani kwamba kutokana na taarifa tuliyonayo, kwamba hatua zinazowekwa (dhidi ya UVIKO-19) kwa ajili ya Michezo hiyo ni kali sana na ni imara sana hatuoni hatari yoyote ya kuongezeka kwa maambukizi katika muktadha huo." ameongeza.

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing itaanza Februari 4 mwaka huu. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha