Mazao ya majini yauzwa vizuri kabla ya Mwaka Mpya wa jadi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 13, 2022
 Mazao ya majini yauzwa vizuri kabla ya Mwaka Mpya wa jadi wa China

Wakati Mwaka Mpya wa jadi wa China unapokaribia kuwadia, uuzaji wa mazao ya majini huko eneo la Fengnan la Mji wa Tangshan wa Mkoa wa Hebei nchini China umeingia kwenye mauzo mazuri kutokana na kuwadia kwa sikukuu. Katika bwawa la samaki la Kijiji cha Mengzhuangzi la Mji mdogo wa Daxinzhuang, wavuvi wanashughulika na kuvuta nyavu na kukusanya samaki ili kukidhi mahitaji ya soko wakati wa kusherehekea sikukuu. Sasa, eneo la ufugaji wa samaki katika eneo hilo linafikia hekta 3,491.3, na mazao ya majini yamefikia tani 56,232 kwa ujumla. (Dong Miaomiao)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha