Maskoti “Bing Dwen Dwen” na “ Shuey Rhon Rhon” wa Michezo ya Olimpiki waonekana Barabara ya Kati mwa Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 13, 2022
Maskoti “Bing Dwen Dwen” na “ Shuey Rhon Rhon” wa Michezo ya Olimpiki waonekana Barabara ya Kati mwa Beijing
(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Picha iliyopigwa Januari 12 ikionesha muonekano wa maskoti “Bing Dwen Dwen” na “Shuey Rhon Rhon” wakiwa katika hatua za mwisho kukamilika.

Sanamu zenye mita 7.5 hivi za “Bing Dwen Dwen” na “Shuey Rhon Rhon”, ambazo ni maskoti rasmi wa Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022, zimeonekana hivi karibuni kwenye Barabara ya Mandhari ya Olimpiki iliyoko mstari wa kati wa Beijing, Mji Mkuu wa China ambao ni mwenyeji wa mashindano hayo ya Olimpiki yanayotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao wa Februari. Muonekano wao mzuri umevutia sana wapita njia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha