Wafanyakazi wa Reli Wafanya Maandalizi kwa pilikapilika za usafari wa Abiria wengi wa Kipindi cha Mwaka Mpya wa Jadi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 17, 2022
Wafanyakazi wa Reli Wafanya Maandalizi kwa pilikapilika za usafari wa Abiria wengi wa Kipindi cha Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Wafanyakazi wa Shirika la Reli la China wakisafisha mabehewa ya treni katika Mji wa Hengyang, Mkoa wa Henan ulioko Katikati mwa China Januari 16, 2022. Pilikapilika za usafari wa abiria wengi katika kipindi cha mwaka mpya wa jadi wa China, mwaka huu zitaanzia Januari 17 na kuendelea hadi Februari 25. Katika kipindi hiki cha usafiri wa abiria wengi wa siku 40 kinachoitwa Chunyun kwa Lugha ya Kichina, Wachina wengi watasafiri kwenda maskani yao kujumuika pamoja na familia zao kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China, na sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China wa 2022 itawadia Februari 1 mwaka huu. (Picha imepigwa na Cao Zhengping/Xinhua)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha