Mlo wa ‘Hotpot’ wa Chongqing wanogesha viungo vya chakula kwa mji huo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 20, 2022
Mlo wa ‘Hotpot’ wa Chongqing wanogesha viungo vya chakula kwa mji huo
Watu wakikusanyika kula mlo wa hotpot karibu na Mto Yangtze katika Wilaya ya Jiulong ya Chongqing, nchini China. [Picha na Liu Song/Kwa China Daima]

CHONGQING – Mji wa Chongqing Kusini-Magharibi mwa China ni maarufu kwa mlo wa hotpot wenye viungo maarufu hususani pilipili. Na inastahili hivyo.

Mlo huo wa hotpot unaweza kupatikana kila mahali. Unahudumiwa pembezoni mwa Mto Yangtze, kwenye misitu iliyo nyuma ya mji huo, kwenye vichochoro na chini ya madaraja ya juu ya barabara, na hata katika baadhi ya ghorofa za chini ya ardhi za majengo ya makazi ya Chongqing zilizoachwa tangu miaka ya 1940, mlo wa hotpot unaongoza upishi wa mji huo.

Mlo huo wa hotpot uligunduliwa kwanza na wapagazi na waendesha mashua waliokuwa wakifanya kazi kando ya Mto Yangtze wakati wa Enzi ya Ming (1368-1644), ambao waliweka vyakula vyote kwenye sufuria moja ya supu ya pilipili, inayochemka, kuwarahisishia kula kwenye boti zao. Kwa sasa mlo huu ni maarufu kote nchini China.

Nyama za kondoo au ng'ombe iliyokatwa vipande vipande vidogo, viungo vya ndani vya wanyama, vyakula vya majini na mboga, karibu vyakula vya aina yoyote vinaweza kupikwa kwenye chungu cha supu ya pilipili hivyo kuufanya Mlo wa Hotpot ya Chongqing kupendwa na kila mtu kwa utamu wake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha