Pilikapilika za mwisho kwa Mbwa wa Doria “Hu Zi”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2022
Pilikapilika za mwisho kwa Mbwa wa Doria “Hu Zi”
Askari wa doria Yu Zhenlong pamoja na Hu Zi wakifanya doria kufuata njia ya Reli ya Harbin-Qiqihar karibu na Kituo cha Daqing Magharibi cha Reli Januari 24. (Picha/Xinhua)

Kwenye njia ya Reli ya Harbin-Qiqihar, ambayo ni reli ya mwendo kasi katika sehemu zenye hali ya baridi kali iliyoko Kaskazini zaidi mwa China, vipo vituo 78 vya kufanya doria, na katika kila kituo kuna askari wa doria watatu na mbwa mmoja wa kufanya doria. Hu Zi ni mbwa wa kufanya doria kwenye njia hiyo ya reli, mwaka huu atastaafu baada ya kumaliza kazi yake ya mwisho ya kufanya doria katika pilikapilika za usafiri wa abiria wengi kipindi cha mwaka mpya wa jadi wa China. Umri wa miaka 14 wa Hu Zi ni sawasawa na umri wa miaka 70 wa binadamu. Mbwa huyu amehudumu kwenye njia hiyo ya reli kwa miaka 7, ambapo kwa jumla amefanya doria ya kilomita elfu 80. Amewasaidia polisi kukamata wahalifu waliotoroka, kuwasaidia wazee waliopotea njia kurudi nyumbani, na kugundua hatari za moto wa mashambani, na kulinda usalama wa reli ya mwendo kasi pamoja na askari wabeba silaha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha