Bahari ya Maua ya Lily yaonekana tena Namibia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2022
Bahari ya Maua ya Lily yaonekana tena Namibia
Watalii wakichuma maua kwenye bahari ya maua ya lily.

Siku za hivi karibuni, kunyesha kwa mvua ya kutosha kuliwezesha bahari ya maua ya lily ionekane tena katika Shamba la Sandhof. Shamba hilo liko mji mdogo wa Malta Hohe, Kusini mwa Namibia ambapo kuna bonde moja, ambapo ni nadra kwa mvua kunyesha huko, na maua ya lily yanaota kwenye shamba la hekta 700 hivi . Lakini katika wakati ambao kuna mvua ya kutosha, ndipo maua yote ya lily yanapoweza kuchanua vizuri , na kipindi cha kuchanua kwa maua ni siku 6 hadi 7 tu. Kama ukikosa fursa, unatakiwa kusubiri kwa miaka kadhaa ili kuiona hali hiyo inayoshangaza ya maua mengi ya lily yanachanua vizuri kwenye shamba kubwa.

Shirika la Habari la China, Xinhua (Mpiga picha: Chen Cheng)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha