

Lugha Nyingine
Vijiji vya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 vyafunguliwa rasmi (3)
BEIJING - Vijiji vya Olimpiki kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 cha eneo la Yanqing, mjini Beijing na Zhangjiakou, Mkoa wa Hebei vilifungua milango yao kwa wanamichezo na maafisa wa timu kwa ajili ya Michezo hiyo siku ya Alhamisi ya wiki hii.
Zhang Guannan, mfanyakazi wa timu ya uendeshaji wa Kijiji cha Olimpiki cha Beijing, amesema kijiji hicho kitawapokea wanamichezo 1,000 na maafisa wa timu kutoka nchi na kanda 44.
Ameongeza kuwa pamoja na huduma bora za malazi, kijiji hicho pia kina vifaa vya mazoezi, burudani na afya ili kukidhi mahitaji ya wanamichezo na viongozi. Jumla ya vyakula 678 vitahudumiwa kwa zamu na baadhi yao ni vyakula maalum kwa ajili ya Mwaka Mpya wa jadi wa China unaotarajiwa hivi karibuni.
Juan Antonio Samaranch Jr., Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki kwa Michezo ya Olimpiki ya Beijing 2022, amepongeza "vifaa vizuri" katika kijiji hicho wakati wa ziara yake, na kuongeza kuwa wanamichezo wana bahati sana kuja kushindana kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 katika mazingira bora na salama.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma