Mapambo ya Mwaka Mpya Yang’arisha Maeneo ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 29, 2022
Mapambo ya Mwaka Mpya Yang’arisha Maeneo ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi
(Picha imepigiwa na He Penglei/Chinanews)

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing itafunguliwa Tarehe 4, Februari, 2022, inakutana kwa majaaliwa na mwaka mpya wa jadi wa chuimilia wa China kwa kalenda ya kilimo ya China. Hivi karibuni, Kijiji cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, kituo kikuu cha vyombo vya habari cha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, hoteli za kutoa huduma kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na sehemu nyingine kadha wa kadha zimepambwa kwa mapambo ya mwaka mpya, popote pale yamebandikwa mapambo ya neno la Kichina “Fu” (maana yake ni baraka), kuning'nizwa taa nyekundu za jadi za China, sanaa za ukataji wa karatasi n.k., ambapo pamejaa hali motomoto ya kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha