Su Yiming apata medali ya dhahabu kwenye mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye theluji kwa kutumia ubao na kuruka hewani kwenye jukwa kubwa kwa wanaume

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 16, 2022
Su Yiming apata medali ya dhahabu kwenye mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye theluji kwa kutumia ubao na kuruka hewani kwenye jukwa kubwa kwa wanaume
Mchezaji wa Timu ya China Su Yiming (Picha/Xinhua)

Februari 15, kwenye fainali ya mchezo wa kuteleza kwa kasi kwenye theluji kwa kutumia ubao na kuruka hewani kwenye jukwaa kubwa kwa wanaume katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, mchezaji wa Timu ya China Su Yiming alitwaa medali ya dhahabu. Hii ni ya medali yake ya pili baada ya kupata medali ya fedha kwenye mchezo wa kuteleza kwenye theluji katika Mteremko kwa ubao kwa Wanaume kwenye michezo hiyo ya Olimpiki. Pia ni medali ya dhahabu ya sita kwa Timu ya China katika awamu hii ya Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, ambayo imeweka rekodi bora zaidi ya idadi ya medali za dhahabu ambazo Timu ya China imewahi kupata kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha