Maji safi kwenye Kijiji cha Uganda yajumuisha watu wa Familia za China na wenyeji wa huko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 16, 2022
Maji safi kwenye Kijiji cha Uganda yajumuisha watu wa Familia za China na wenyeji wa huko
Katika Kijiji cha Bukasa cha Wilaya ya Wakiso katikati mwa Uganda, mama huyu mjamzito akichota maji kutoka kwenye kisima kipya kilichozawadiwa na Mfuko wa Uhisani wa Wachina waishio nchini Uganda, Februari 12, 2022, . (Xinhua/Zhang Gaiping)

Hivi karibuni, katika Kijiji cha Bukasa, Wilaya ya Wakiso ya katikati mwa Uganda, wanakijiji wanakwenda kwenye kisima kipya kuchota maji. Maji safi yanatiririka bila kusita kutoka kwenye bomba kutoka hodhi la maji ya kisima hicho.

Huko nyuma, maji ya kunywa ya wanakijiji hao yalitoka kwenye kisima kifupi kilichochimbwa kwa mikono, ambacho kiko mbali na makazi yao na ilichukua muda mrefu kupanga foleni ili kuchota maji. Baada ya utekelezaji wa mradi wa kuchimba visima na kusambaza maji wa Mfuko wa Uhisani wa Wachina waishio Uganda katika Kijiji cha Bukasa, wanavijiji zaidi ya elfu kumi sasa wanaweza kunywa maji safi.

Mwanakijiji Emmanuel Masaba alisema, hivi sasa familia yake inaweza kupata maji safi bila ya wasiwasi wa kuambukizwa magonjwa, hivyo wanaweza kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kwa matibabu.

Takwimu kutoka Wizara ya Maji na Mazingira ya Uganda zinasema, katika nchi hiyo takribani asilimia 30 ya watu wanatumia maji yanayochotwa kutoka visima vifupi, mabwawa, mito na maziwa, na kushindwa kupata maji safi ya kunywa. Takwimu za Wizara ya Afya ya Uganda zinaonesha, kila siku mamia ya watu katika nchi hiyo wanakufa kwa ugonjwa wa kuhara damu, kipindupindu na magonjwa mengine kadha wa kadha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha