

Lugha Nyingine
Maambukizi ya UVIKO-19 yapungua, soko la maua la Kenya lafufuka
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 16, 2022
Tarehe 14, Februari, kwenye soko la maua nchini Kenya, kulikuwa na msururu usioisha wa wakazi wengi waliokwenda kununua maua, na wauzaji wa maua pia walikuwa na pilikapilika .
Maua ya Kenya siyo tu yanapendwa na wakazi wa nchi hiyo, bali pia ni maarufu sana duniani. Ikiwa mojawapo ya nchi kubwa zaidi za kuuza maua kwenye soko la kimataifa, Kenya inapanda aina zaidi ya 100 za maua.
Sambamba na maambukizi ya UVIKO-19 duniani, biashara ya maua ya Kenya inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika miaka ya hivi karibuni. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Maua nchini Kenya Clement Tulezi alisema, anatarajia kuimarika kwa soko la maua hivi karibuni, kunaweza kubadilisha hali ya kudidimia ya biashara hiyo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma