Dereva wa Basi ambaye ni Mjumbe wa Bunge la Umma la China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 01, 2022
Dereva wa Basi ambaye ni Mjumbe wa Bunge la Umma la China
Wang Yan akizungumzia utumiaji wa vifaa vya kuchaji katika vituo vya mabasi pamoja na mwakilishi kutoka Kampuni ya Umeme ya Taifa ya Huduma ya Magari yanayotumia umeme Tawi la Tianjin kwenye chumba cha mkutano cha ofisi ya huduma ya basi huko Tianjin, Feb 24, 2022.

Dereva wa basi wa Tianjin Wang Yan ni mjumbe wa Bunge la Umma la China (NPC). Tangu aanze majukumu yake Mwaka 2018, Wang ameendelea kuwasilisha maoni na mapendekezo kwa NPC, ambayo yanahusu mawasiliano na huduma za matibabu na afya.

Wang akiwa dereva wa basi, anasikiliza maoni ya abiria wake, na kujumuisha maoni yao yanayoweza kuwa na ushawishi kwa sera za serikali.

Mwaka huu ni mwaka wa mwisho wa kipindi chake cha kuwa mjumbe wa Bunge la Umma la China, Wang atawasilisha maoni na mapendekezo yake kuhusu kuongeza vifaa vya kuchaji magari ya kutumia umeme katika maeneo ya huduma ya barabara kuu. (Xinhua/Sun Fanyue)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha