

Lugha Nyingine
Biashara kati ya China na Afrika yafikia kiwango cha juu zaidi Mwaka 2021, ikionyesha uimara wakati wa Janga la UVIKO-19 (3)
![]() |
Picha iliyopigwa Septemba 1, 2021 ikionyesha eneo la ujenzi wa mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe huko Harare, Zimbabwe. (Picha na Wanda/Xinhua) |
NAIROBI - Biashara kati ya China na Afrika imeondoa mwelekeo wa kudorora kwa uchumi wa Dunia, na wachambuzi wanaamini kuwa imechangia katika kuimarika kwa uchumi wa Afrika katika kukabiliana na changamoto za UVIKO-19.
Mshirika mwenzi Mkuu wa Kibiashara
China imesalia kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 12 mfululizo. Kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na Idara Kuu ya Forodha ya China, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na Afrika Mwaka 2021 ilifikia dola za kimarekani bilioni 254.3, ikiwa ni ongezeko la asilimia 35.3 ikilinganishwa na Mwaka 2020, ambapo kati ya thamani hiyo, bidhaa za Afrika zilizouzwa nchini China imefikia dola bilioni 105.9, ikiwa ni ongezeko la asilimia 43.7 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Swiss-African Business Circle iliyotolewa Februari, 2022 China imedumisha nafasi yake ya kuwa mwekezaji mkubwa zaidi barani Afrika kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Kukua kiuchumi pamoja na China
Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa la (UNCTAD) linaamini kuwa kuimarika kwa uchumi wa Afrika Mwaka 2021 kulichangiwa zaidi na kuboreshwa kwa mazingira ya kibiashara ya nje, hasa uungaji mkono wa dhati wa China na masoko mengine ambayo yaliimarisha uwezo wa Afrika wa kuuza bidhaa nje. Ukuaji wa biashara barani Afrika pia umeungwa mkono na bei ya juu ya bidhaa kwenye masoko ya kimataifa.
Ripoti ya Swiss-African Business Circle inasema, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, China ilitengeneza wastani wa nafasi za ajira 18,562 kwa mwaka barani Afrika na nafasi hizo za ajira zimekuwa zikiongezeka kwa kila mwaka.
Msukumo katika kufufua uchumi
"Kwa sasa, nchi duniani kote bado zinakabiliwa na kazi mbili ngumu za kuzuia na kudhibiti mlipuko wa virusi vya korona na kufufua uchumi. Maendeleo ya kiwango cha juu ya uchumi wa China yametoa msukumo na imani kwa ajili ya kufufua uchumi wa Dunia na Afrika," anasema Chen Mingjian, Balozi wa China nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), Pato la Taifa la China (GDP) lilichangia asilimia 18 ya uchumi wa Dunia Mwaka 2021, na mchango wake katika maendeleo ya uchumi wa Dunia umekuwa ukiongezeka kwa kasi mwaka baada ya mwaka.
Wakati huo huo, ukuaji thabiti wa uchumi wa China pia unaleta fursa zaidi za maendeleo katika kuinua uchumi wa nchi za Afrika.
"Mwaka 2021, ikilinganishwa na mwaka uliopita, mauzo ya Ethiopia nchini China yaliongezeka kwa asilimia 8; uwekezaji mpya wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) kutoka makampuni ya China kwenda Ethiopia uliongezeka kwa asilimia 346; jumla ya thamani ya miradi mipya iliyotiwa saini na makampuni ya China nchini Ethiopia iliongezeka kwa asilimia 25," anasema Zhao Zhiyuan, Balozi wa China nchini Ethiopia.
Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja (BRI) vimekuwa na mchango mkubwa katika ushirikiano kati ya China na Afrika.
Kwa mujibu wa ripoti ya Taasisi ya Sera ya Afrika, tangu BRI ilipopendekezwa Mwaka 2013, China imesaidia miradi ya kisasa ya miundombinu kama vile reli, barabara, bandari, mabwawa, viwanda na mawasiliano ya kidijitali, na kuingiza uhai katika ukuaji wa uchumi wa Kenya.
Mkurugenzi wa Kituo cha Masomo kuhusu China katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania, Humphrey Moshi anasema, "FOCAC iliyoanzishwa Mwaka 2000 ni kuendeleza na kuimarisha urafiki kati ya China na Afrika na inatoa uhakikisho kwa uhusiano wa hali ya juu kati ya China na Afrika katika karne mpya."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma