Habari yako,Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi!

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 02, 2022
Habari yako,Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi!
Kivutio cha Kileta bahati “Shuey Rhon Rhon” cha Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi kwenye uwanja wa kutunuku medali wa Zhangjiakou. Picha ilipigwa Februari 28.

Kadiri siku ya kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi inavyokaribia, ndivyo mji wa Beijing unavyokamilisha maandalizi yake ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi baada ya kufungwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi. Kileta bahati “Bing Dwen Dwen kimepambwa popote badala ya Kileta bahati “Shuey Rhon Rhon” kikisubiri kuwakaribisha wanamichezo wa nchi mbalimbali watakaoshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi.

 Ili kuwawezesha walemavu kushiriki kwenye michezo ya mashindano, kufanya kazi zao na kutazama michezo bila matatizo wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi, idadi ya vifaa na miundombinu isiyo na vikwazo kwa walemavu imeongezwa na kukarabatiwa katika maeneo matatu ya mashindano ya Beijing, Yanqing na Zhanjiakou, na uhakika wa utoaji wa huduma umezingatiwa kwa makini.

Mpiga picha: Mou Yu/ Shirika la Habari la China Xinhua

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha