

Lugha Nyingine
Sherehe za Ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 zafanyika Beijing
Sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 zimefanyika leo usiku katika Uwanja wa Michezo wa Taifa wa China. Rais Xi Jinping wa China na Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Walemavu ya Kimataifa Parsons wamehudhuria ufunguzi huo.
Ufunguzi huo ulianzia saa mbili usiku, na sherehe zake zina sehemu 12, zikiwemo maandamano ya wanamichezo na kuwasha mwenge wa Michezo ya Olimipiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi.
Sherehe zinazoelekea ufunguzi rasmi zenye kaulimbiu ya “kutia moyo” zina sehemu mbili, za kukumbuka historia ya Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi na kuongeza uelewa juu ya moyo wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu.
Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing itafanyika kuanzia leo mpaka tarehe 13, Machi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma