Wajumbe wa Bunge la Umma la China watoa mapendekezo 487 kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2022
Wajumbe wa Bunge la Umma la China watoa mapendekezo 487 kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma
Wafanyakazi wa sekretarieti ya Mkutano wa Tano wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC) wakichambua mapendekezo kutoka kwa wajumbe wa NPC mjini Beijing Machi 9, 2022. (Xinhua/Li Xin)

BEIJING - Wajumbe wa Bunge la Umma la 13 la China (NPC) walikuwa wamewasilisha mapendekezo 487 kufikia saa sita mchana siku ya Jumanne wiki hii, ambayo ni tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maoni na mapendekezo katika Mkutano wa Tano wa NPC ya 13 unaoendelea hapa Beijing, imesema sekretarieti ya mkutano huo.

Sekretarieti hiyo imesema pia imepokea takriban maoni ya kiujenzi na ya kukosoa yapatayo 8,000, kutoka kwa wajumbe wa Bunge la Umma la China .

Mapendekezo mengi yanahusu kuharakisha kutunga sheria kuhusu nishati, uchumi wa kidijitali, elimu ya shule ya awali, malezi ya wazee, na kulinda haki na maslahi ya wanawake.

Wajumbe wa Bunge la Umma pia wametoa mapendekezo kuhusu kuendeleza ustawishaji vijijini, kukuza maendeleo mazuri ya uchumi wa kidijitali, na kukabiliana na utekaji nyara na usafirishaji haramu wa wanawake na watoto.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha