Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing yafungwa

(CRI Online) Machi 14, 2022
Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing yafungwa
Rais Xi Jinping wa China akipunga mkono katika sherehe ya ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 kwenye Uwanja wa Taifa wa Beijing, Machi 13, 2022. (Xinhua/Xie Huanchi)

Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing imefungwa jana usiku katika Uwanja wa michezo wa Taifa mjini Beijing, na rais Xi Jinping wa China na rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki ya Walemavu, Andrew Parsons wameshiriki kwenye sherehe ya ufungaji wa michezo hiyo.

Katika siku 9 zilizopita, wanamichezo karibu 600 kutoka nchi na sehemu 46 wameshindana kwenye uwanja wa michezo na kuonyesha moyo wa kujitegemea na kujiendeleza.

Bw. Parsons amepongeza michezo hiyo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing ambayo amesema imefanyika kwa usalama, uaminifu na murua , na kuweka kiwango kwa Michezo mingine ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Walemavu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha