

Lugha Nyingine
Timu ya Waenezi wa utekelezaji wa sheria kwa kupanda farasi (3)
![]() |
Timu ya huduma ya uenezi utekelezaji wa sheria ya “Nyota ya Mbuga” ya Wilaya ya Ruoergai ya Mkoa wa Sichuan. (Picha kutoka Polisi wa Mkoa wa Sichuan) |
Siku chache zilizopita, polisi wa Timu ya Huduma ya uenezi wa utekelezaji wa sheria “Nyota ya Mbuga” ya Idara ya Usalama wa Umma ya Wilaya ya Ruoergai ya Tarafa inayojiendesha ya makabila ya Watibet na Waqiang ya Aba katika Mkoa wa Sichuan waliendesha magari na kupanda farasi kwenda nyumbani kwa wakazi wa huko kueneza utekelezaji wa sheria kwa kupitia shughuli za aina mbalimbali zinazoweza kupokewa na wakazi wa huko.
Inafahamika kwamba, ukubwa wa jumla wa eneo la Wilaya ya Ruoergai ni zaidi ya kilomita 10000 za mraba na nyumba za wakulima na wafugaji zinatapakaa huko me. Ili kuwawezesha watu wanaoishi katikati ya milima, ambao ni wenye kiwango cha chini cha kusoma na kuandika na wasioelewa lugha ya Kichina wajifunze na kufuata sheria na kutumia silaha ya kisheria kujilinda, Idara ya Usalama wa Umma ya Wilaya ya Ruoergai imeunda Timu ya huduma ya uenezi wa utekelezaji wa sheria “Nyota ya Mbuga” ambayo inaundwa na polisi wengi watekelezaji wa sheria, pamoja na polisi wanaotoka vikosi vya usimamizi wa usalama wa jamii, na wengine wa Polisi wa Makosa ya Jinai, Polisi wa Trafiki na polisi wa Misitu, ambao wote ni wanaojua kuongea kwa lugha ya Kichina na Kitibet, na ni uti wa mgongo katika uenezi wa utekelezaji wa sheria.
Ili kupata matokeo mazuri ya uenezi, polisi hao walipofafanua waliunganisha vifungu vya sheria na matukio yaliyotokea kwenye eneo hilo, ili wafugaji wapate ujuzi wa sheria kwa kupitia “kusikiliza hadithi” na kuelewa kwa kina vitendo vya kuvunja sheria na uhalifu vinavyoweza kuleta madhara mabaya ya namna gani kwa watu binafsi na familia zao. Kwa wale walioko mbali sana na si rahisi kufika kusikiliza uenezi wa utekelezaji wa sheria, polisi wanaweza kwenda nyumbani kwao kwa hiari.
Tangu Timu hiyo iundwe Mwezi Oktoba, Mwaka 2020, Idara ya Usalama wa Umma ya Wilaya ya Ruoergai imetoa huduma ya uenezi wa utekelezaji wa sheria kwa maelfu ya familia katika makazi na vijiji 91, tarafa 6 na miji midogo 7 katika Wilaya ya Ruoergai ikilenga makundi mbalimbali ya watu. Ilifanya vizuri uenezi wa utekelezaji wa sheria zaidi ya mara 230 kwa watu zaidi ya elfu thelathini, na kusaidia kuongeza uelewa juu ya utekelezaji wa sheria miongoni mwa wakulima na wafugaji, ambapo matukio mbalimbali ya kwenda nyuma ya sheria na vitendo vya uhalifu yamepungua kwa asilimia 10 katika wilaya hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma