Mandhari nzuri ya Majira ya Mchipuko kama picha iliyochorwa kwenye Kijiji cha watu waliohamishwa kwa ajili ya kupunguza umaskini huko Chongqing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 18, 2022
Mandhari nzuri ya Majira ya Mchipuko kama picha iliyochorwa kwenye Kijiji cha watu waliohamishwa kwa ajili ya kupunguza umaskini huko Chongqing
Maua yaliyochanua yakionesha mandhari nzuri ya majira ya mchipuko kwenye Kijiji cha Zhongyuan cha watu waliohamishwa kwa ajili ya kupunguza umaskini katika Mji wa wilaya wa Shihui wa Eneo la Qianjiang la Mji wa Chongqing.

Katika kazi ya kuwasaidia watu kujiendeleza na kuondokana na umaskini, serikali ya Eneo la Qianjiang ilitekeleza mradi wa kuwahamisha watu wa Kijiji kizima cha Zhongyuan kwenye mahali pengine, ambapo familia 78 za wanavijiji walioishi kwenye mlima mrefu wamehamishwa kwenye sehemu mpya iliyokamilishwa miundombinu ya maji, umeme, barabara, maeneo ya kufanya mazoezi na kadhalika. Wakati huohuo, serikali ilitekeleza mipango ya shughuli za kiuchumi zinazofaa kwa wanavijiji hawa, ambapo ilianzisha kituo cha kilimo, kupanda stroberi kwenye mashamba na shughuli nyingine. (Mpiga picha: Yang Min/ Tovuti ya Picha ya Umma)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha