Rwanda yafanya Tamasha la Wushu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2022
Rwanda yafanya Tamasha la Wushu
Shirikisho la Kungfu-Wushu la Rwanda Jumamosi iliyopita ilionesha maonesho mbalimbali za Kungfu za China ili kuhimiza mshikamano wa wanachama wake. (Picha/Xinhua)

Shirikisho la Kungfu-Wushu la Rwanda Jumamosi iliyopita lilitoa maonesho mbalimbali ya Kungfu ya China ili kuhimiza mshikamano wa wanachama wake.

Wachezaji Kungfu wa Rwanda, wakiwemo watu wazima na watoto, walifurahisha watu wote kwa michezo mbalimbali ya Kungfu kama vile Tai Chi na Wing Chun katika Uwanja wa Kigali.

Licha ya Kungfu, watu kutoka mashirikisho mengine pia walionesha michezo mingine ya Wushu, kama vile taekwondo, karate, judo na masumbwi.

Marc Uwiragiye, mkuu wa shirikisho hilo alipohojiwa na mwandishi habari wa Shirika la habari la Xinhua, China alisema, “leo, tunafanya maonesho kwenye tamasha hilo ili kuhimiza mshikamano na ushirikiano wa watu wote wanaopenda Wushu nchini Rwanda. Wushu ni alama ya mshikamano wa wanachama wetu.”

Aliongeza kuwa, “tamasha hilo lina umuhimu mkubwa sana kwa sisi Wanyarwanda, na tunapaswa kuonesha kwa dunia kuwa tuko pamoja tunaweza kuhimiza maendeleo endelevu kwa kupitia Wushu.” 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha