

Lugha Nyingine
Kituo cha Uzalishaji bidhaa nchini China chajizatiti kuleta utulivu wa minyororo ya ugavi bidhaa katikati ya mlipuko mpya wa UVIKO-19
![]() |
Mfanyakazi akinyunyizia dawa za kuua virusi ndani ya basi huko Futian mji wa Shenzhen, katika Mkoa wa Guangdong, nchini China Machi 13, 2022. (Picha na Chu Yan/Xinhua) |
SHENZHEN - Wakati kuzuka upya maambukizi ya UVIKO-19 hivi karibuni kunapunguza kasi ya maisha ya kawaida katika Delta ya Mto Zhujiang ya China, juhudi za pamoja zinafanywa ili kuhakikisha utulivu wa mnyororo wa ugavi bidhaa katika eneo hilo.
Mamlaka na makampuni ya kanda hiyo, ambayo ni kituo cha uzalishaji wa bidhaa wa China, zimetekeleza hatua kadhaa ili kupunguza athari za mlipuko wa janga wa hivi karibuni kwenye shughuli za uzalishaji na biashara.
Maamuzi makini na hatua za haraka
Katika mji wa Kusini mwa China Shenzhen, hatua kali na za uangalifu za kuzuia na kudhibiti janga la UVIKO-19 zimetekelezwa tangu Machi 13 ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Korona.
Hatua hizo ni pamoja na kusimamisha usafiri wa mabasi na treni za chini ya ardhi.
Kwa mujibu wa makao makuu ya idara ya kuzuia na kudhibiti UVIKO-19 ya Shenzhen, maeneo ya umma na yale ya viwanda yaliwekwa chini ya usimamizi uliofungwa.
Hatua kali kama hizo za kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona zimethibitishwa kuwa zenye ufanisi na kusaidia kuzuia kuenea kwa maambukizi ya UVIKO-19, na hivyo kuhakikisha kurejea kwa maisha ya kawaida.
Viongozi wa serikali wa eneo hilo wamesema, kando na kurejea kwa maisha ya kawaida, ofisi za serikali, kampuni, na biashara huko Shenzhen zimepangwa kuanza tena kazi za kawaida na uzalishaji kuanzia leo Jumatatu wakati maambukizi ya UVIKO-19 ya hivi karibuni yakipungua.
Kulinda Minyororo ya Ugavi
Katika Kiwanda cha Kampuni ya New Industries Biomedical Engineering (Snibe) katika Wilaya ya Pingshan ya Shenzhen, zaidi ya wafanyakazi 1,300 waliishi na kufanya kazi chini ya usimamizi uliofungwa ili kudumisha uzalishaji wa kawaida wa bidhaa wakati wa mlipuko wa virusi vya Korona wa hivi karibuni.
Snibe ni kampuni ya kuzalisha bidhaa za tiba inayojikita katika zana za maabara za vipimo na vifaa vya upimaji, ikitoa bidhaa kwa zaidi ya mashirika 7,700 ya matibabu nchini China na kuuza kwa nchi na maeneo 147 duniani.
"Ili kuhakikisha huduma za upimaji afya zinazofanywa na mashirika zaidi ya 20,000 ya matibabu duniani kote, kampuni yetu ilizishinda changamoto na kuendelea na uzalishaji wetu," Ding Chenliu, Naibu Meneja Mkuu wa Snibe amesema.
Snibe ni moja tu ya kampuni katika eneo hilo ambazo zimejitahidi kuhakikisha uzalishaji huku kukiwa na kuibuka tena kwa UVIKO-19.
Katika eneo la viwanda visivyo na uchafuzi kwa mazingira vya vifungashio na uchapishaji la Luk Ka katika Kitongoji cha Qiaotou katika Mji wa Dongguan, Mkoa wa Guangdong nchini China, serikali ya eneo hilo ilianzisha maeneo ya muda ya kupima virusi vya Korona ili kutoa huduma za upimaji kwa wafanyakazi karibu 2,000 kutoka zaidi ya makampuni 30 katika eneo hilo.
Viongozi wa serikali za mitaa pia waliongoza maeneo hayo ya viwanda kupitia usimamizi wake uliofungwa na utoaji wa nyaraka za kuruhusu kuingia na kutoka kwa viwanda vyenye mahitaji ya usafirishaji, wakifanya kila juhudi kuhakikisha udhibiti wa UVIIKO-19 huku wakilinda na kudumisha shughuli za uzalishaji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma