Ufufukaji mpya wa “Mto Mama” wa Mkoa wa Hainan, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 22, 2022
Ufufukaji mpya wa “Mto Mama” wa Mkoa wa Hainan, China
Picha iliyopigwa kutoka angani Machi 19, 2022 ikionesha mandhari ya Bustani ya Ardhi Oevu ya Fengxiang ambapo Mto Meishe unapita katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. (Xinhua)

Ukiwa umepewa jina la “Mto Mama” wa Haikou, Mto wa Meishe hivi karibuni uliwekwa na Wizara ya Maji ya China kwenye orodha ya “mito 11 ya maskani ya watu ya kuvutia zaidi kote nchini ”.

Mto huo wenye urefu wa kilomita 16, unatiririka kwenye sehemu kubwa kupita eneo la mji la Haikou. Kabla ya miaka ya 1990, mto huo ulikuwa na maji safi na wa kuvutia, lakini kutokana na maendeleo ya uchumi na ongezeko la idadi ya watu, ulibadilika kuwa mto uliochafuliwa sana. Kwa sababu ya harufu yake mbaya, wakazi walioishi karibu nao waliogopa kufungua madirisha, hali hiyo ilisababisha wakazi wengi wahame eneo hilo.

Mwaka 2016, mradi wa kushughulikia maji yaliyochafuliwa ulioweka mkazo katika urejesho wa mazingira ya asili na kuboresha maisha ya watu ulileta matumaini.

Mji huo kwanza ulitekeleza utaratibu wa kuweka mkuu wa mto kwenye sehemu mojamoja ya mtiririko wa mto katika Mkoa wa Hainan, na utaratibu huu ulisaidia sana kushughulikia uchafu wa maji ya mto, na kuhakikisha utekelezaji mzuri wa hatua za kurejesha mazingira ya asili.

Baada ya jitihada za miaka mingi, Mto Meishe umepata uhai tena.

Mji wa Haikou utaongoza katika Kampeni ya Kubana matumizi ya maji i ya Mkoa wa Hainan, na hivi sasa miradi 217 yenye uwekezaji wa Yuan bilioni 36.6 (takribani Dola za Marekani bilioni 5.8) imepangwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha