Kisanduku cheusi cha pili cha ndege ya China iliyoanguka chagunduliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 28, 2022
Kisanduku cheusi cha pili cha ndege ya China iliyoanguka chagunduliwa
Picha iliyopigwa Machi 27, 2022 ikionesha kisanduku cheusi cha pili kilichogunduliwa katika sehemu ya ajali ya ndege katika wilaya ya Tengxian ya Mkoa wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua)

Makao makuu ya kitaifa ya kukabiliana na hali ya dharura yalithibitisha kugunduliwa Jumapili iliyopita kwa kisanduku cheusi cha pili cha ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la China Eastern Airlines iliyoanguka Jumatatu wiki iliyopita mkoani Guangxi kusini mwa China.

Mkurugenzi wa Ofisi ya Usalama wa Usafiri wa Ndege katika Idara Kuu ya Usafiri wa Ndege za Abiria ya China Zhu Tao katika mkutano na waandishi wa habari wa Jumapili iliyopita alisema, kisanduku cheusi cha pili kimetambuliwa na wachunguzi kuwa ni chombo cha rekodi ya data za usafiri wa ndege, na kimepelekwa kwa maabara kwa ajili ya kusimbuliwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha