Rais Xi Jinping wa China apanda miti kwa mwaka wa 10 mfululizo akiwa kiongozi mkuu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 31, 2022
Rais Xi Jinping wa China apanda miti kwa mwaka wa 10 mfululizo akiwa kiongozi mkuu
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, akipanda mti wakati wa shughuli ya upandaji miti katika Eneo la Daxing, mjini Beijing, Machi 30, 2022. Viongozi wengine akiwemo Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Wang Huning, Zhao Leji, Han Zheng na Wang Qishan pia walishiriki kwenye shughuli hiyo. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Rais wa China, Xi Jinping Jumatano wiki hii amepanda miti katika mwaka wa 10 mfululizo wa ushiriki wake kama kiongozi mkuu katika shughuli ya kila mwaka ya upandaji miti katika Mji Mkuu wa China, Beijing.

Rais Xi, amesema amekuwa akishiriki shughuli hiyo ili kutoa mchango wake katika ujenzi wa China nzuri na kuwapa moyo watu wa jamii nzima, haswa vijana kuhimiza maendeleo ya kiikolojia ili mazingira ya China yawe bora zaidi.

Viongozi wengine akiwemo Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Wang Huning, Zhao Leji, Han Zheng na Wang Qishan pia walishiriki kwenye shughuli hiyo.

Viongozi hao wamepanda miti kwa pamoja na watu kutoka Beijing kwenye bustani ya mji katika eneo la Daxing, Kusini mwa Beijing.

Wakati akipanda miche ya aina mbalimbali ya miti, Xi aliwauliza watoto wa shule waliokuwa karibu naye kuhusu masomo yao, akawatia motisha kukuza hisia ya kufanya kazi kwa bidii, na kuwaambia waongeze uelewa wao juu ya kulinda mazingira ya asili na kutunza rasilimali.

Rais Xi pia amehimiza juhudi zinazoendelea na ngumu za kulinda na kurejesha mfumo wa mazingira ya asili na kufikia uboreshaji wa kimsingi wa mazingira.

Juhudi katika usimamizi wa tabianchi duniani

Akibainisha kuwa misitu ni muhimu kwa kuhifadhi maji, kupata faida za kiuchumi, na kulinda usalama wa nafaka, Xi amesisitiza kwamba jukumu lake muhimu kama nyenzo ya kufyonza kaboni inapaswa pia kuthaminiwa.

Xi amesema Misitu na nyanda za majani zina jukumu la msingi na la kimkakati katika usalama wa kiikolojia na ameongeza kuwa misitu na nyanda zinazostawi ni muhimu kwa mfumo mzuri wa ikolojia.

“Hivi sasa, ustaarabu wa ikolojia nchini China umeingia katika kipindi muhimu cha kuboresha mazingira” Xi amesema, akitoa wito wa utekelezaji usioyumba wa mawazo mapya ya maendeleo na kufuata njia ya kuweka kipaumbele katika uhifadhi wa ikolojia na kukuza maendeleo ya kijani.

Rais Xi ametoa wito kwa juhudi za kuratibu ulinzi na usimamizi wa kimfumo wa milima, mito, misitu, mashamba, maziwa, nyasi na ardhi ya mchanga, kuendeleza upandaji miti wa kisayansi, kuongeza wingi na ubora wa rasilimali za misitu na nyasi, na kuunganisha na kuimarisha uwezo wa ikolojia wa kunyonya kaboni.

“Kwa kufanya hivyo, tutatoa mchango mkubwa zaidi katika usimamizi wa mazingira na tabianchi duniani, na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa kwa ajili ya binadamu kuishi kwenye hali ya kupatana na mazingira ya asili.” amesema Xi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha