Mji huu mdogo utakuwa Ukumbi wa Kukaribisha Wageni wa Kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2022
Mji huu mdogo utakuwa Ukumbi wa Kukaribisha Wageni wa Kimataifa
(Picha inatoka China News.)

Tarehe 30, katika Mji wa Tunxi wa Mkoa wa Anhui, China, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi aliendesha mkutano wa tatu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi jirani za Afghanistan, na kwa kufuata, mazungumzo kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa “Afghanistan na nchi jirani zake” pia yalifanyika katika mji huo.

Kihalisi, tokea zaidi ya siku kumi zilizopita, mambo ya kidiplomasia yameshaanza kufanyika mfululizo huko wakati wa majira ya mchipuko. Kutoka tarehe 19 hadi 20, Machi, Bw. Wang Yi alikuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia na wa Algeria waliowasili hapa China, na pia kufanya mkutano kwa kupitia video pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania. Mji mdogo Tunxi umekuwa ukumbi wa kuwakaribisha wageni wa kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kwa nini mambo muhimu ya kidiplomasia yamefanyika huko Tunxi, ambao ni mji mdogo ulioko chini ya Mlima Huangshan?

Viongozi wa China waliwahi kukaribisha wageni kutoka nchi mbalimbali katika sehemu nyingi nje ya Beijing, ambapo sehemu hizo zilisifiwa sana na wageni. Katika sehemu hizo za Kusini au Kaskazini mwa China, mbali na kufanya mambo ya kidiplomasia, wageni kutoka nchi mbalimbali duniani pia wamejionea mandhari nzuri na mila na desturi mbalimbali nchini China.

Mji wa Tunxi uko chini ya Mlima Huangshan, ambao ni mali ya urithi wa utamaduni na maliasili ya Dunia, na Mto Xin‘an unatiririka kupitia mji huo pia. Kwenye Mlima Huangshan kuna mti maarufu sana unaoitwa “Msonobari wa Kukaribisha Wageni”, ambao umekuwa kama ni alama ya shirikishi na uchangamfu na ukarimu walionao watu wa China. Kwenye ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing uliofanyika siku chache zilizopita, fashifashi iliyopigwa yenye muundo wa msonobari huo ilioneshwa juu ya Uwanja wa Michezo wa Taifa wa China, Wachina walitumia njia yao pekee ya mahaba kwa kuwakaribisha wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani. Katika historia, kutokana na shughuli za biashara zilizoendelea vizuri, Tunxi ilikuwa kituo cha utamaduni wa eneo la Huizhou – Katika miaka 400 iliyopita, wafanyabiashara wa Anhui waliendeleza shughuli zao za biashara kutoka eneo hilo hadi sehemu za Asia ya Kusini Mashariki, Japan na Ulaya. Eneo hilo linaonesha sifa ya Wachina wanaofanya juhudi za kujiendeleza siku hadi siku..

Hivi sasa, mambo mengi zaidi ya kidiplomasia yanafanyika katika miji midogo kama Tunxi. Miji hiyo midogo ina hadithi nyingi za kuvutia, miji midogo hiyo imeshuhudia mambo ya kidiplomasia ya nchi kubwa. Wakati wageni wa nchi mbalimbali walipowasili miji hiyo, walijionea utamaduni na mila na desturi mbalimbali wa China, zaidi walijionea maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha