Mabaki ya Ngome ya Keyakekuduke ya Xinjiang, China yaorodheshwa kwenye orodha ya magunduzi 10 muhimu zaidi ya mabaki ya kale (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 01, 2022
Mabaki ya Ngome ya Keyakekuduke ya Xinjiang, China yaorodheshwa kwenye orodha ya magunduzi 10 muhimu zaidi ya mabaki ya kale
Picha kutoka kwenye faili ikionesha sehemu ya silaha iliyogunduliwa katika mabaki ya Ngome ya Keyakekuduke yaliyoko Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur wa Kaskazini Magharibi mwa China. (Picha/Xinhua)

Mabaki ya Ngome ya Keyakekuduke iliyoko Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur wa Kaskazini Magharibi mwa China yameorodheshwa kwenye orodha ya magunduzi 10 muhimu zaidi ya mabaki ya kale ya China ambayo yalitangazwa Alhamisi wiki hii.

Kiongozi wa timu ya mradi wa kufukuliwa kwa mabaki hayo ya kale Hu Xingjun, ambaye anatoka taasisi ya utafiti wa mabaki ya kale ya utamaduni ya eneo hilo alisema, mnara huo ulifanyika katika jangwa lililoko kilomita 90 Kusini Mashariki mwa Wilaya ya Yuli ya Eneo linalojiendesha la Mongolian Bayingolin, unatoka Enzi ya Tang (618-907).

Taasisi hiyo imefanya kazi ya kufukua ili kutafiti mabaki ya kale katika eneo la mita za mraba 2300 kuanzia mwaka 2019 hadi 2021, na iligundua nyumba za wakazi, nyuzio za mbao, ngazi za kibanda, marundo ya majivu, dimbwi na mabaki ya kale zaidi ya 1400 zikiwemo nyaraka za karatasi.

Hu alisema, kazi ya kufukuliwa kwa ngome hiyo inasaidia kugundua muonekano halisi wa ngome hiyo, na kutoa data nyingi zenye ushahidi wa kweli kwa ajili ya utafiti wa ngome za kijeshi za mipakani katika zama za kale za China.

“Nyaraka hizo pia zimethibitisha usimamizi wenye ufanisi wa serikali kuu ya Enzi ya Tang kwa maeneo ya Magharibi,” Hu aliongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha