

Lugha Nyingine
Madaktari wa China wafanyia upasuaji kwa watoto wenye mdomo wazi Zanzibar
(CRI Online) April 05, 2022
Awamu ya 31 ya kikosi cha matibabu cha China visiwani Zanzibar imefanya shughuli ya “Malaika Tabasamu”, na kuwafanyia upasuaji watoto 40 waliozaliwa na tatizo la mdomo wazi kuanzia tarehe 28 Machi hadi tarehe 2 Aprili. Mkuu wa hospitali ya Mnazi Mmoja ya Zanzibar Marijali Msafiri amesema, shughuli hii siyo tu inaondoa ugonjwa wa kimwili, bali pia inasaidia watoto kuondoa tatizo la kisaikolojia, ambalo lina umuhimu mkubwa kwa afya yao katika siku za usoni. Daktari wa China Chen Hongsheng amesema, mpaka sasa hali ya watoto inaendelea vizuri, na baadhi yao wametoka hospitali. Ameongeza kuwa, madaktari wa China wataendelea kuwafuatilia na kuwapatia matibabu ya baadaye.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma