Upendo wa dhati wakati wa maisha ya kujitenga kijamii kutokana na korona (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 06, 2022
Upendo wa dhati wakati wa maisha ya kujitenga kijamii kutokana na korona
Mtu anayejitolea Weng Yaosheng (kushoto) akiwasaidia wazee kusafisha chumba Tarehe 5, Aprili. (Xinhua)

Katika familia zaidi ya 1600 za wakazi wa makazi ya Jinlvxincheng ya eneo la Putuo, Shanghai, wako wazee wengi wasioishi pamoja na watoto wao. Wakati wa kujitenga kijamii na kukabiliana na janga la korona , maisha ya wazee hao yanakabiliwa na changamoto nyingi. Kwa hivyo watu wanaojitolea wanawasaidia wazee hao kufanya kazi mbalimbali, kama vile kuwapelekea chakula, kuwasaidia kupimwa, kusafisha nyumba zao, na kutoa msaada wa kisaikolojia. Katika wakati huu usio wa kawaida, watu hao wanaojitolea wanawapa wazee faraja kila siku, wakiwasaidia wazee hao kupunguza wasiwasi na msongo wa mawazo. Mtu anayejitolea Weng Yaosheng alisema, “kama tukiweza kuwasaidia wazee hao hata hawana haja ya kutembea zaidi kwa miguu, kazi zetu zimekuwa na umuhimu.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha