

Lugha Nyingine
Majukwaa ya Maduka ya Mtandaoni yasaidia usambazaji wa kila siku wakati wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona huko Shanghai (8)
![]() |
Wahudumu wakifungasha chakula kwenye mifuko kwa ajili ya oda za mtandaoni katika duka la chakula huko Shanghai, Mashariki mwa China, Aprili 10, 2022. (Xinhua/Chen Jianli) |
Idadi inayoongezeka ya Kampuni kubwa za maduka ya mtandaoni na majukwaa ya upelekaji wa chakula yamejiunga na vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona aina ya Omicron huko Shanghai, ili kuhakikisha usambazaji wa mahitaji ya kila siku ya jiji hilo.
Mamlaka ya mji huo Jumapili yalithibitisha kuwa, kampuni kubwa za maduka ya mtandaoni kama vile JD.com, majukwaa ya upelekaji wa chakula kama vile Meituan na Eleme, pamoja na kampuni za huduma ya upelekaji zimeshirikiana na mji huo, ili kutoa mahitaji ya kila siku wa wakazi huko.
Ukiwa na idadi ya watu ya milioni 25, Shanghai hivi sasa umekuwa uwanja mkuu wa kupambana na maambukizi ya virusi vya korona. Jumapili ya wiki iliyopita umeripoti watu walioambukizwa virusi vya korona zaidi ya 20,000. Mji huo umechukua mkakati wa usimamizi wa kujifunga kwa muda, na kufanya raundi kadhaa za upimaji wa virusi vya korona mjini kote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma