Picha: Mfereji Mkubwa wa Jinghang (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 15, 2022
Picha: Mfereji Mkubwa wa Jinghang

Mfereji Mkuu wa Jinghang ni mfereji mrefu zaidi uliochimbwa na binadamu duniani. Mfereji huo unatoka Mji wa Hangzhou wa Mkoa wa Zhejiang, Kusini mwa China, hadi Mji wa Beijing wa Kaskazini mwa China, na urefu wake kwa jumla umefikia kilomita 1790.

Mfereji mkuu huo ulianza kujengwa wakati wa Kipindi cha Spring na Autumn katika zama za kale za China, na ulifanyiwa ukarabati mkubwa wakati wa Enzi ya Sui. Hadi sasa historia yake imefikia zaidi ya miaka 2000.

Mfereji huo umefanya kazi kubwa kwa ajili ya maendeleo na mabadilishano ya kiuchumi na kitamaduni kati ya sehemu za kusini na za kaskazini za China, na umetoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa kilimo na viwanda ya maeneo yaliyo karibu na mfereji huo.

Picha inkionesha sehemu ya Beijing-Tongzhou ya Mfereji Mkuu wa Jinghang. Juni, 2021, sehemu ya Beijing ya Mfereji mkubwa wa Jinghang yenye urefu wa kilomita 40 ilianza rasmi kupitika kwa meli za utalii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha