

Lugha Nyingine
Barabara iliyojengwa na kampuni ya China yawanufaisha watu wa Rwanda
![]() |
Tarehe 21, Aprili, mfanyakazi akichora mstari wa alama kwenye barabara ya Huye inayoeleka Kibeho, Rwanda. (Picha/Xinhua) |
Katika Mkoa wa Kusini wa Rwanda, barabara ya lami iliyo ya tambarare, ambayo ni barabara ya magari ya kupishana, ikionekana kama inatambaa na kuzunguka njia ya vipengele vya vilima vingi kwa kufuata barabara hiyo iliyojengwa milimani, barabara hiyo inaunganisha miji ya Huye, Kibeho, Ngoma n.k.
Barabara hiyo ina urefu wa kilomita 66, na ilisasishwa na kukarabatiwa na Kampuni ya Miradi ya Umeme na Maji ya China. Sasa njia kuu ya barabara hiyo imezinduliwa kimsingi.
Mkazi mmoja wa Mji wa Huye alimwambia mwandishi wa habari kuwa, “Hali ya barabara ilikuwa mbaya sana, safari ya kutoka Huye mpaka Ngoma kwa gari kwa kawaida ilichukua masaa matatu , ambapo ilikuwa na miteremko mingi njiani. Baada ya kukarabatiwa, safari hiyo inachukua dakika 40 tu, na imeleta mabadiliko makubwa kwa maisha yetu.”
Ukiwa mmoja wa miradi ya ushirikiano wa Rwanda na China wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, mradi wa kusasishwa na kukarabatiwa kwa barabara hiyo ulianzishwa Aprili, 2019, na uliahirishwa kukamilika hadi Oktoba, 2022 kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya korona.
Meneja wa mradi huu Yao Zheng alisema, Mkoa wa Kusini ni sehemeu muhimu ya kuzalisha chai ya milima mirefu, na hali bora ya barabara inaweza kuongeza uuzaji wa nje wa chai ya aina hii, kuhimiza maendeleo ya uchumi, na kuboresha maisha ya wakazi.
Katika kipindi chake cha ujenzi wa pilikapilika, mradi huo uliwaajiri wafanyakazi wenyeji zaidi ya 600, na umewaandaa wafanyakazi wengi wenye teknolojia za kuendesha mashine. Fundi mmoja wa upimaji wa mradi huu alisema, barabara hii inaleta uhai na ustawi kwa vijiji vilivyoko pembezoni mwake .
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma